Wazazi peke yao wanahusika na malezi ya watoto wao? watoto wanasikitisha, wamekuwa watukutu, hawawatii wazazi wao. Kizazi hiki tunahitaji watoto wenye hofu ya Mungu, tuanze kuwafundisha watoto wetu Mungu ni nani, yuko wapi, anapenda nini na kazi zake ni zipi. Pia tuwape majina mazuri ambayo yataenda na tabia zao. Na wazazi nao tubadilike, tusifuate dunia inavyoenda, tutaathiri watoto na vizazi vyetu.
โMlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzeeโ โ Mithali 22:6
Filed under: NENO
